Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - DURU YA WANAWAKE WA MWANZO KATIKA KUSOMA NA KUENEZA ELIMU
Posted: Mon Jan 19, 2026 2:56 am
*Legacy Post Number 77 from MediaSwahili
Topic: Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - DURU YA WANAWAKE WA MWANZO KATIKA KUSOMA NA KUENEZA ELIMU
Timeline: 2013-03-09 17:42:01
Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa
“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”
Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - DURU YA WANAWAKE WA MWANZO KATIKA KUSOMA NA KUENEZA ELIMU
(Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)
Kilichochapishwa Na Daarul Arqam,
Chapa Ya Pili,
DURU YA WANAWAKE WA MWANZO KATIKA KUSOMA NA KUENEZA ELIMU
Hakika duru ya mwanamke Muislamu katika historia ya Uislamu, historia ya Da‘wah na historia ya mataifa na watu imesajili upeo wa ubora, utukufu na utakaso katika nyaraka. Sote tunajua na kuelewa yale aliyoyafanya Mama wa Waumini Bibi ‘Aishah bint Abubakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) katika kuhifadhi Hadithi nyingi pamoja na kuzisomesha. Huyu bibi mtukufu alikuwa anaulizwa maswali mengi na wakubwa miongoni mwa Masahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) katika mambo mengi ya dini.
Historia ya Kiislamu imesajili kwa herufi za nuru na dhahabu majina ya Sahabiyat watukufu (Radhiya Allaahu ‘anhum) mfano wa Asmaa bint Abubakr, Umm ‘Atiyyah al-Ansariyah, Umm Kabshah Qadha‘iyah, Asmaa bint ‘Umays, Umm Sulaym bint Milhan, Umm Dardaa na fatimah bint Qays (Radhiya Allaahu ‘anha), wote walikuwa wapokezi na waalimu wa Hadithi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kulikuwa na mwanamke amabaye alikusanya Qur-aan.
’Allamah Sh. Dkt. Yusuf al-Qaradhawi anatuelezea:
“Al-Hafidh Jamalud Deen as-Suyuty amemtaja mwanamke aliyekusanya Qur’ani lakini hajahadithia hayo mtu yeyote.
Naye ni Umm Waraqah bint ‘AbdAllaah bin al-Harith (Radhiya Allaahu ‘anhu). Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikumwa akimzuru na kumuita Shaheedah.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuamuru asalishe watu wa nyumbani kwake na alikuwa na muadhini. Aliuliwa na kijana aliyekuwa mtumwa wake wakati wa Ukhalifa wa ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu).
hapo ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema, ‘Amesema kweli Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye alikuwa akisema: Twende pamoja tumzuru (tumtembelee) Shaheedah”.
Tunaporudia majina ya wanawake Muhaddithaat wa kipindi cha Tabi‘in tutaona majina mengi. Miongoni mwao ni Fatimah bint Siirin, Zaynab bint al-Muhajir, Safiyyah bint Shaybah, ‘Aishah bint Sa‘d bin Abi Waqqas na wengineo.
Imaam Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake pekee ametoa idadi inayafikia wanawake hamsini.
Na huko Cordoba, Spain (wakati wa utawala wa Waioslamu baina ya 711 - 1492) kulikuwa na takriban Mafakihi wa kike sitini miongoni mwa Mafakihi wa Kiislamu ambao walishughulika kutoa Fatwa.
Katika nyumba zao waliekewa taa. Taa hizo zilikuwa haziwekwi ila katika nyumba za watu wa Fatwa na Fikihi.
Alikuwa Fatimah bint Muhammad bin Ahmad as-Samarqandi mwandishi wa “Tuhfatul Fuqahaa” ambaye alipata elimu na ufahamu mikononi mwa babake.
Alihifadhi Tuhfah na akaolewa na ‘Alaad Deen bin Abubakr mwandishi wa “Al-Badai‘”.
Mumewe alikuwa akikosea naye akimrekebisha. Fatwa zilikuwa zikija na zinapotolewa nje zilikuwa na hati yake na ya babake.
Alipoolewa Fatwa zikawa zinatoka na hati yake kwenye karatasi, hati ya babake na mumewe.
Wakati wa Sa‘eed bin al-Musayyab, Tabi‘i mkubwa na mtukufu aliyeteswa kwa misimamo yake katika kipindi cha utawala wa Bani Umayyah.
‘Abdul-Maalik bin Marwan, Khalifa wa tano wa dola hiyo alikwenda kumposea mwanane binti ya Sa‘eed ambaye alikataa.
Baadae Sa‘eed alimuoza bintiye mwanafunzi wake aliyekuwa masikini lakini mchaji Allaah.
Baada ya harusi, mume alikuwa anataka kila wakati kwenda kusoma kwa mwalimu na baba mkwe lakini mkewe alikuwa anamwambia kaa hapa nami nitakufundisha elimu ya Sa‘eed.
Aliandika Abu Muslim al-Farahiidi mtaalamu wa Hadithi juu ya wanawake sabiini waliokuwa huru na watumwa ambao walishindana katika nyanja ya Tarbiyah (malezi).
Mwandishi wa msabaka huo alikuwa mwanamke ambaye alihadithia katika karne ya sita Hijri na sauti ikawa inasikika kwa mbali na halaiki ya watu.
Ni mambo gani ambayo yamefanya wanawake Waislamu wasifikie mifano ya mabibi hawa watukufu? Hasa tukiangalia kuwa sisi tunaishi katika vita vigumu na mapambano yasiyomalizika. Mapambano dhidi ya vita vya kifikra za Msalaba (Manasara) na hujumu kali na ya kukinaisha kutoka kwa Uzeyuni wa Kimataifa na Ujamaa (Ukomunisti) wa kilimwengu juu ya Uislamu na Waislamu katika kila sehemu na Pembe zote za dunia.
Maadui wote hawa wanawafanyia Waislamu ubaya na kuonyesha kuwa Uislamu na wafuasi wake ni mdudu adui wa wanawake na elimu.
Kuongezea yale wanayo yachapisha kwa kutoa Maelezo mabaya dhidi ya Uislamu na kueneza Misingi yenye kuua na kuvunja.
**{Legacy activities, comments etc counter: 3870; topic series: 5; forum: MediaSwahili; associated: 5- /*}